VIBAKA WAWILI WACHOMWA MOTO KAHAMA BAADA YA KUIBA COMPUTER...!!
Watu wawili ambao
hawajafahamika majina yao wameuwawa kwa kuchomwa moto na wananchi wanaozaniwa kuwa na hasira
kali katika kijiji cha Kagongwa wilayani
Kahama Mkoani Shinyanga baada ya kudaiwa
kuiba vitu mbalimbali ikiwemo Komputa.
Tukio hilo limetokea
leo majira ya saa tano asubuhi baada ya
watuhumiwa hao kujaribu kuwakimbia viongozi wa Sungusungu waliokuwa
wanawashikilia baada ya kuwakamata....
Kwa mujibu wa Mashuhuda
wamesema vijana hao walikuwa ni tishio katika mji huo kutokana na kuiba
marakwamara hivyo wananchi baada ya kuwakamata wameamua kuwachoma moto kwa
madai kuwa iwe ni fundisho kwa wengine.
Wamesema Awali watuhumiwa
walikamatwa na sungusungu ya kijiji cha Iponya wilayani humo Kabla ya kuamriwa
wakaoneshe vitu hivyo ndipo wakapata mwanya wa kukimbia.
Diwani wa kata ya Kagongwa
Hamis Kashantole Ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata
hiyo amekataa kuzungumzia tukio hilo kwa madai kwamba hana muda wa kuongea.
Jeshi la polisi wilayani Kahama
limethibitisha kutoikea kwa tukio hilo na hadi sasa linaendelea na uchunguzi.
0 comments: