SHEIKH MKUU WA MKOA WA MARA OTHMAN MAGEE AFARIKI DUNIA


 
Taarifa tulizozipata hivi punde toka chanzo chetu makini zinasema kuwa aliyekuwa Sheikh mkuu wa mkoa wa Mara Othman Magee,amefariki dunia usiku huu akiwa katika matibabu hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam ambako alikuwa amelazwa akisumbuliwa na saratani ya kibofu. 

Awali marehemu Sheikh Othman Magee alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando na ugonjwa ulipomzidia alihamishiwa Muhimbili.

Shughuli mbalimbali na taratibu za mazishi zimeanza kufanyika nyumbani kwake mtaa wa Kennedy kata ya Mviringo, Musoma mjini ambapo mazishi yanategemewa kufanyika kesho kutwa mjini humo.
 
INNALILLAHIWAINNAILAIHIROJIUN.

0 comments: