WAZEE WA KIJIJI(WANANZENGO) WAGOMEA KUZIKA MAITI ..HUKO KAHAMA SHINYANGA

               marehemu .Bakar omar(papa mukulu)

Katika hali isiyo ya kawaida wazee wa kitongoji cha malunga kata ya malunga wilayani kahama mkoani shinyanga, leo wamegoma kuzika mwili wa Bakari Omari-(Papa Mukulu) (40) mkazi wa eneo hilo aliyefariki usiku wa kuamkia leo.

Sakata hilo limetokea kufuatia uamzi wa wazee hao kuwazuia vijana wa eneo hilo pamoja na marafiki zake kumzika Omari wakidai faini kwakuwa alikuwa haudhurii misiba hali iliyosababisha vyombo vya usalama kuingilia kati.



                                 


Kwa upande wake rafiki wa karibu wa marehemu Omari Salum Juma amesema, mtafaruku huo umesababishwa na wazee hao kutaka faini kubwa yaani ng’ombe mmoja  au mbuzi watano au pesa taslim shilling 250,000 viitu hambavyo havikuweza kupatikana.
Kufuatia rafiki zake Omari ambaye hakuwa na familia wala ndugu wa karibu kukosa uwezo wa kumtolea marehemu faini hiyo,waliwaomba wazee wawapunguzie na hatimaye wakaruhusiwa kulipa shilingi 50,000=
Marehemu Omari anayesadikiwa kuwa ni raia wa Kongo ameingia nchini 1989 KWA KILE kilichodaiwa kutafuta maisha, alikuwa akifanyakazi ya kubeba mizigo katika mashine za KUKOBOA mpunga mjini kahama.
Marehemu amezikwa leo jioni katika makaburi ya malunga kahama,huku rafiki zake waliomlipia faini wakiwa hawana jibu la kuwa faini hiyo inakwenda wapi.

wananzengo wakiandaa kaburi kwa ajili ya mazishi

safari ya kuelekea

wakina mama wakiwa msibani hapo.



chanzo-Bongo na matukio blog.


0 comments: