YALIVYOKUWA MAZISHI YA MSANII WA KUNDI LA UIGIZAJI KOMEDI LA FUTUHI MZEE DUDE LEO JIJINI MWANZA.


Dua ya kuuombea kheri mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa kundi la uchekeshaji wa luninga la FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa jina la Mzee Dude ilifanyika majira ya saa 9:00 nyumbani kwake Ilemela jijini Mwanza ikiwa kabla ya mazishi yaliyofanyika leo jioni majira ya saa 10:00.
Awali kabla sala maalum ilifanyika.
Waigizaji mbalimbali wa sanaa mbalimbali wameshiriki akiwepo Mc. Katumba ambaye anaonekana akiwa na wasanii wa kundi la BABATAN Itagata, Kafuku Kahualanga na Mwanshum ambao walifanya kazi na marehemu kwenye kundi la FUTUHI (kabla hawajajiengua) na wa kwanza kulia ni Tatu wa FUTUHI.
Ni wakati wa kuusitiri mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa kundi la uchekeshaji wa luninga la FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa jina la Mzee Dude, katika makaburi ya Iloganzala wilayani Ilemela jijini Mwanza.


Kwa mapenzi mema na urafiki hata watoto wadogo walishiriki kuweka mchanga kuusitiri mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa kundi la uchekeshaji wa luninga la FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa jina la Mzee Dude aliyefariki jana jioni majira ya saa 11 hivi.

Katika mazishi hayo Beat Agenda iliwakilishwa naye DVJ Bavon (mwenye skafu na kofia kushoto).
Shekhe wa wilaya ya Ilemela Shk. Mohamed Yusufu akitoa neno la barka kwa waliohudhuria mazishi ya aliyekuwa mwigizaji wa kundi la uchekeshaji wa luninga la FUTUHI marehemu Omary Majuto al maarufu kwa jina la Mzee Dude
Dj John Lyatow wa Club Villa akiwa na wadau wengine walioifahamu kazi ya marehemu.
Baadhi ya watoto wa marehemu wakijumuika na wajukuu na marafiki wengine wa marehemu katika sala ya kuhitimisha maziko kifamilia.
Kumbukumbu za Brothers

0 comments: