BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND, PENNY AELEZEA AINA YA MWANAUME ANAYEMTAKA
Penniel Mwingila aka VJ Penny ambaye wengi wanamfahamu kama
mpenzi wa mkali wa Bongo Flava, Diamond Platinumz ambao hivi sasa hawako
pamoja, anaamini kuwa ingawa hakuna mwanaume mkamilifu, kuna sehemu
yupo mkamilifu japo kwa kiasi kidogo.
Penny amefunguka katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo5
kuhusu maisha yake kwa ujumla na uhusiano wake na Diamond Platinumz
ambaye hivi karibuni ameonekana kurudiana na mpenzi wake wa zamani ‘Wema
Sepetu’.
Msichana huyo mrembo alisema bado hajafikiria kuwa na mwanaume
mwingine, “bado, si kwamba sitongozwi, wanaume wanakuja lakini
najaribu…hakuna mwanaume mkamilifu, najaribu kutafuta mwanaume anayeweza
kuwa mkamilifu kidogo najua yuko sehemu.”
Penny ambaye hivi sasa maisha yake yako kwenye spotlight akifuatiliwa
na kuandikwa kila anapofanya jambo, hali iliyosababishwa na kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na Diamond, amedai kuwa anatamani arudie maisha
yake ya zamani ambayo yalikuwa ni maisha ya faragha.
“Napenda kurejea kwenye maisha niliyokuwa nayo, it was much fun, napenda maisha yangu ya faragha.” Penny ameuambia mtandao huo.
Akizungumzia kuhusu kinachoendelea hivi sasa kati yake na Diamond
amesema alihisi anahitaji kumpa nafasi mwimbaji huyo, na kwamba hadi
sasa wawili hao wamepeana nafasi ili kila mmoja afanye mambo yake.
“Kama uhusisiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu
wanaachana kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi,
wote ni vijana na wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya,
kuona kipi hasa unachokihitaji katika maisha. Unajua ukimruhusu ndege
afanye vitu mbalimbali then unajua kama ‘mti huu ndio unanifaa, mti huu
haunifai’. Hivyo nilihisi wote tulihitaji hicho, tulihitaji space hivyo
nikampa nafasi na mimi kuchukua nafasi.”
Amedai kuwa alipoona picha za Diamond akiwa na Wema Sepetu,
alishituka kama watu wengine walivyokuwa surprised lakini alipomuuliza
Diamond alimwambia walikuwa wanafanya ‘movie’. Mrembo huyo bado
anaisubiri movie ya Diamond na Wema Sepetu.
Hata hivyo, Penny amedai kuwa mwaka huu anahitaji kujikita zaidi
katika kufanya kazi yake, na kwamba anaamini utakuwa mwaka wa ushindi
kwake.
Source: Bongo5.com
0 comments: