Kamati ya Ardhi,Maliasili na Mazingira watembelea hifadhi ya taifa ya Mkomazi.


 Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi maliasili na mazingira Mh James Lembeli akiwa ameongozana na naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Mahamud Mgimwa wakisalimiana na wafanyakazi wa hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi.

 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, maliasili na mazingira wakitembelea eneo la mradi wa kufuga faru pamoja na Mbwa Mwitu.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi,maliasili na mazingira,pamoja na viongozi wa hifadhi ya taifa ,TANAPA wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la WTPF,  linalosimamia mradi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi,Tony Fitzjohn (Kushoto)
 Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira James Lembeli akiteta jambo na Mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn kabla ya kuembelea eneo maalumu linalotumika kuhifadhi Faru.
 Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira, James Lembeli,Mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn,Naibu waziri wa maliasili na utalii  Mahamud Mgimbwa wakiwa kwenye gari maalumu tayari
kwenda kujionea mradi wa Faru.

 Mbwa mwitu wakiwa wamehifadhiwa katika maeneo maalumu ndani ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi kabla ya kuachiwa kwenda porini.
 Mbwa mwitu wakiwa wamehifadhiwa katika maeneo maalumu ndani ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi kabla ya kuachiwa kwenda porini.
 Baadhi ya vifaa ambavyo vimekuwa vikitumika katika mradi wa Faru katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi ambavyo ni sehemu ya vinavyodaiwa kutozwa kodi  na serikali licha ya kwamba hutumika katika mradi wa Faru ambao pia ni wa serikali.
 Naibu waziri wa maliasili na mazingira ,Mahamud Mgimwa akiwa amemshika mtoto wa Tembo katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi,wengine ni mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na Mazingira James Lembeli na
mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn. 



Naibu waziri wa maliasili na mazingira ,Mahamud Mgimwa akiwa amemshika
mtoto wa Tembo katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi,wengine ni
mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na Mazingira James Lembeli na
mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi

0 comments: