HATARI SANA...!! Fisi wafukua na kuila miili ya Vibaka wawili waliouwawa na kuchomwa moto na Wananchi Wilayani Kahama...!!
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida wananchi wa kijiji cha Iponya
kata ya Kagongwa Wilayani Kahama Mkoani Shinyinga wamelazimika kuzika upya
mabaki ya Marehemu wawili waliozikwa wiki iliyopita baada ya leo kukuta
wamefukuliwa na Fisi.
Miili hiyo ni ya watu wawili ambao walisadikiwa kuwa vibaka waliuwawa na
wananchi wenye hasira kali na kuchomwa moto na kisha kuzikwa katika makaburi yaliyopo katika kijiji
hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda
wakizungumza redio kahama fm
wamesema hali hiyo imetokana na kuzikwa
katika makaburi ambayo hayana kina kirefu hivyo wanyama hao kuwa rahisi
kwao kufukua na kuanza kula maiti hizo....
Mmoja wa mashuhuda Hasan
Msoma amesema waligundua kutokana na wao
kufika katika maeneo ya makaburi kwa lengo la kuzika Mtoto ndipo wakaona mabaki
ya miili ya marehemu huku eneo kubwa la miili ikiwa imeliwa na fisi.
Amesema baada ya kuona hali hiyo waliutaarifu uongozi
wa kata ambao ulifika na kushiriki katika
mazishi na kusema kuwa haki za
binadamu hazikuzingatiwa katika kuzika
watu hao kwani walifukiwa katika shimu lenye kina kifupi cha futi moja.
0 comments: