MAUAJI..!! MME ACHINJA MKE WAKE KAMA KUKU, BAADA YA KUNYIMWA TENDO LA NDOA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA...!
!
Mkazi
wa mmoja mkazi wa kijiji cha Tazengwa wilaya ya Nzega, mkoani Tabora,
Juma Kiyabo (45) amemchinja mke wake, Wande Monera (34), kabla ya
mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika
jaribio la kutaka kujiua.
Tukio
hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16
mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba
mara kwa mara.
Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kaunga alisema taarifa za awali
zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara
kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo
mbaya.
Kamanda
Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye
alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake
lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.
Credit-Kandili yetu blog

0 comments: