MTOTO AOKOTWA AKIWA AMEKATWA MAPANGA...!!
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.
| Mtoto Ismail Barihegi. |
Stori: Makongoro Oging’
MTOTO Ismail Barihegi, mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kijiji cha Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ameokotwa akiwa amekatwa mapanga baada ya kudaiwa kuipeleka mifugo yao katika mashamba.
MTOTO Ismail Barihegi, mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kijiji cha Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ameokotwa akiwa amekatwa mapanga baada ya kudaiwa kuipeleka mifugo yao katika mashamba.
Barihegi
ambaye amelazwa katika Jengo la Mwaisela Wodi na 17, Muhimbili,
alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba siku ya tukio
(hakumbuki)alikuwa akichunga ng’ombe porini lakini ghafla walitokea
watu na kumwuliza kwa nini aliwaachia ng’ombe wake kufika shambani.
Alisema
aliwakatalia watu hao kwamba mifugo iliyokuwa shambani haikuwa ya
kwao, na hata kuwaonesha ng’ombe wao, lakini watu hao hawakumwelewa.
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.
“Wenye
ng’ombe walishakimbia, waliniambia ni lazima waniue, niliwaomba
wasiniue, lakini hawakunijali, niliishiwa nguvu, damu nyingi ilikuwa
imenitoka,waliondoka na kuniacha porini peke yangu.
“Nilipiga
kelele ili nipate msaada lakini hakuna aliyejitokeza, nilikata tamaa,
baada ya saa kadhaa mtu mmoja alipita na kuniona, akawaita watu akiwemo
Mwenyekiti wa kijiji chetu, wakaja kunichukua na kunikimbiza katika
zahanati,” alisema mtoto huyo.
Kijana
huyo alisema kwamba baada ya huduma ya kwanza katika zahanati hiyo,
alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuonekana
mbaya zaidi na kwamba ana uhakika wazazi wake hawajui alipo kwani hadi
sasa hawajafika kumtembelea.
“Ninamshukuru
sana mwenyekiti kwa kunipa msaada mkubwa, sasa hivi amerudi kijijini,
najua atawapa taarifa ndugu zangu, ninawashukuru madaktari na wauguzi
kwa kuokoa maisha yangu kwani kwa sasa nina nafuu tofauti na
nilivyookotwa katika msitu mnene,” alisema Barihegi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, Athumani mtasha alipoulizwa kuhusiana na tukio alisema kuwa amehamishiwa makao makuu.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, SACP Urich matei yupo nje ya mkoa kikazi ila kaahidi kufuatilia sakata hilo kwa undani.
CREDIT: GPL
CREDIT: GPL
0 comments: