TAZAMA MTOTO HUYU ANAVYOTESEKA NA KANSA YA JICHO.

Mtoto Neema Joseph kutoka Bulungwa mwenye umri wa miaka miwili akisumbuliwa na kansa ya jicho akiwa na mama yake katika viwanja vya halmashauri ya Mji Kahama  katika kampeni za upimaji wa kansa ya shingo ya uzazi kwa kina mama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akifungua kampeni hizo juzi katika uwanja wa Halmashauri ya Mji Wilayani hapo
Benson amewataka wanaume kutowazuia wake zao pindi wanapotaka kwenda kupima afya  zao ili wabaini tatizo  mapem ana kupema tiba kwa muda muafaka.

Pia amewataka wanawake wa Wilaya ya Kahama kuwahi mapema katika vituo vya afya mara wanapoona dalili za awali za kansa,Kwa sababu tatizo hili limeonekana kuwa ni chanzo cha vifo vingi kwa kina mama nchini.

Katika kampeni hizo  Wanawake 201 walijitokeza kupima saratani ya Shingo ya kizazi kwa siku mbili tarehe 28 na 29 machi 2014. taklibani wanawake 17 wamekutwa na dalili za awali za Saratani ambayo ni sawa na 8.5%,.

Mganga mkuu wa Hospitali ya mji wa Kahama Dr. Helen Membe akimchunguza kwa makini Mtoto huyo, ambapo alimuamuru akae katika hospitali ya kahama huku wakiendelea na uchunguzi wa jicho hilo na jitihada za B. Membe za kumpeleka katika hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza zinaendelea.

Mkurugenzi wa Shirika la HUHESO FOUNDATION Juma  Mwesigwa ambaye ameshirikiana na wataalamu wa Hospital ya Wilaya ya Kahama kutoa huduma hiyo ya Upimaji.





0 comments: