Balaa jingine Geita!! KIJANA AJINYONGA HADI KUFA KWENYE CHOO CHA MAMA MKWE WAKE,ALITAKA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE AKAKIMBIWA NA MKEWE
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daudi James(33) mkazi wa mtaa wa Shilabela mjini Geita mkoani Geita amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni kwa mama mkwe wake kwa kutumia kitenge.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Daud James amekutwa amejinyonga chooni kwa mama mkwe wake eneo la General Tyre.
Akizungumzia tukio hilo mama mkwe wa marehemu Lucia Magulu(32) amesema marehemu alimuoa binti yake Dorothea Jacksoni(18) mwaka
mmoja uliopita huku akiwa na ujauzito wa mwanamme mwingine na baada ya
kujifungua wameendelea kuishi na mtoto wao ambaye ni Hellena mwenye umri
wa miezi kumi.
Akiendelea
kusimulia mkasa huo amesema binti yake Dorothea Jacksoni(18) walikuwa
wamehitlafiana na mme wake na kurudi nyumbani takribani zaidi ya mwezi
mmoja kwa sababu za marehemu mme wake kuwa anamutaka mkewe wafanye tendo
la ndoa kinyume na maumbile ndicho kilichomfanya arudi nyumbani.
"Jana jioni alipofika hapa nyumbani alikaa
hadi walipomaliza kula chakula cha jioni na alipoambiwa arudi nyumbani
kwake Shilabela alikataa na kutaka aende na mke wake ",anaeleza mama
mkwe.
"Baadae
mke wake alipomkatalia kwenda marehemu alimuomba kitenge mke wake kwa
maelezo ya kuwa anaenda kulala kwa rafiki zake na ndipo alipopewa,cha
kushangaza na kusikitisha leo asubuhi tumemkuta kajinyonga kwa kitenge
hicho chooni",ameongeza mama mkwe.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa
uchunguzi bado unaendelea ili kubaini sababu gani zilipelekea kifo chake.
Hata
hivyo kamanda Konyo ameitaka jamii kuacha mambo ya kujichukulia maamuzi
ya kujiua bila sababu za msingi huku akiwataka waandishi wa habari nao
kuelimisha jamii iachane na tabia za kujinyonga kila mara wanapokuwa
wamezozana na wake zao.
Hili
ni tukio la pili kutokea ndani ya siku tatu ambapo juzi mkazi wa
tambukareli mjini Geita alijinyonga na kijining’iniza kwenye mti wa
mpera baada ya kuhitlafiana na mke wake.
Na Valence Robert wa Malunde1 Blog -Geita
0 comments: