Unyama uliopitiliza!! MTOTO AFUNGIWA KWENYE BOKSI KWA MIAKA MINNE HUKO MOROGORO
Askari Polisi wa Kike ( kushoto) ambaye jina lake hakikuweza kufahamika
mara moja akimwesha juisi ,mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne
Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box kwa miaka 4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria . |
Mwanamke
aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege,
Morogoro juzi alishushiwa kipigo na wananchi kutokana na kumficha mtoto
wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa
miaka minne.Tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi baada ya majirani
zake kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia
Zongo kuhusu mtoto huyo, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu
akiwa na umri wa miezi tisa.
Zongo alisema majirani hao walimweleza pia kuwa jirani yao huyo
hamfanyii usafi mtoto huyo wala kumtoa nje.Baada ya kupata taarifa hizo,
Zongo alimtafuta Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana
naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa
akijibu kwa kubabaika.
Moja ya maswali aliyoulizwa ni idadi ya watoto wake na akajibu kuwa ana wawili lakini wakati akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa, hivyo kuwapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasra akiwa ndani ya boksi.
Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo ndani ya nyumba, kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo na kumlazimu mtendaji kutoa taarifa polisi.
Akijibu maswali ya polisi, mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na umri wa miezi tisa baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia mwaka 2010.Pia mtuhumiwa alikiri kwamba mtoto huyo hajawahi kupewa chanjo yoyote wala kupelekwa kliniki.akitoa maelezo hayo huku akiwa amemshikilia mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo alizokuwa akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho alimwogesha Julai mwaka jana.
Pia alisema alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa nyuma ya mlango wa chumba.

0 comments: