KAMA ULIKUWA HUJUI LEO NI HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI, HAKUNA KIINGILIO, KILA MTU RUKSA KUSHIRIKI
MBUNGE
wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia
kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga
lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani
ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya
Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kwamba hakuna kadi.
"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!" alisema Nassari.
Nasari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .


0 comments: