MBUNGE VICKY KAMATA AELEZEA SAKATA LA NDOA YAKE KUTOFUNGWA
Mwanamuziki wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake
kudaiwa kuzuiliwa kufungwa kutokana na kudaiwa mwanaume aliyetaka
kufunga naye ndoa ana ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo
zilikuwa ni habari za kutungwa na hazikuwa na ukweli wowote.
Vicky amesema jana kuwa maneno mengi ambayo
yalikuwa yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofungwa yalikuwa
yametengenezwa na watu.
“Kweli ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja
na hayo mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa hajaruhusu kuwa
tarehe 24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.
"Mimi kama binadamu
na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga vinginevyo , kwaiyo siku
zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya binadamu.
"Ni
kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba
waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka
2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo
bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.
"Kuhusu swala la kwamba alikuwa na mke
wake , mke wake alikwenda kuzuia Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale
yalikuwa tu ni maneno ambayo yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa
interest zao ,lakini siyo kwamba nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu hata
kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba
wangu aliongea na vyombo vya habari akasema mimi sijaenda Dodoma wala
sijaenda kuzuia harusi.
"Kwaiyo maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke
wake amezuia yalikuwa ni maneno ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao
wenyewe lakini siyo kweli.
"Kuhusu kwamba hajulikani alipo mimi hilo
siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba yupo na anaendelea na shughuli
zake kama kawaida, kama ambavyo mimi naendelea na shughuli zangu kama
kawaida, tunawasiliana, yani cha kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa
basi.
"Hata kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini
mungu ndo mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo
kama Mungu alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na
binadamu mwingine hataki bado ingefungwa...
"Kwaiyo mimi sitaki kuamini
sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu wamechangia kwa kiasi
kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi ninaamini ni mapenzi ya Mungu tu
yametimizwa kwa staili hiyo” Alisema Vicky

0 comments: