MASIKINI..!! WALE MAPACHA WALIOTENGANISHWA, MMOJA UTUMBO WAKE UPO NJE

Mama wa watoto mapacha Eliud na Elikana, Grace Joel akiwa amempakata mtoto Eliud ambaye kwa sasa anasumbulia na tatizo la kutokwa na utumbo. Picha na Godfrey Kahango
 
 Suala la matibabu ya mtoto mmoja kati ya pacha waliotenganishwa nchini India baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana, limechukua sura mpya baada ya mganga mkuu wa Wilaya ya Kyela, Festo Dugange kusema hajawahi kusikia wala kumwona mtoto aliyetoka utumbo kukataliwa kutibiwa hospitalini kwake.

Dugange alitoa kauli hiyo kutokana na wazazi wa watoto hao kuiambia Mwananchi kwamba mtoto Eliud anaumwa na utumbo wake upo nje na kwamba alifika Hospitali ya Wilaya ya Kyela lakini hakupatiwa matibabu kwani daktari alimweleza kwamba anatakiwa asubiri kwenda India tu.

Mtoto Eliud na mwenzake Elikana walizaliwa Februari 20,2013 wilayani Kyela wakiwa wameungana maeneo ya kiunoni hali iliyoilazimu Serikali kuwapeleka nchini India ambako walitenganishwa na madaktari bingwa kwa njia ya upasuaji.

Walirejea nchini  na kufikia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hata hivyo siku chache baada ya watoto hao kurejea kijijini kwao Kasumulu maarufu kwa jina la Juakali wilayani Kyela, hali ya Eliud iliaanza kubadilika baada ya sehemu kubwa ya utumbo wake mpana kutokeza nje ya mwili.
Mama wa watoto mapacha Eliud na Elikana, Grace Joel akiwa amempakata mtoto Eliud ambaye kwa sasa anasumbulia na tatizo la kutokwa na utumbo. Picha na Godfrey Kahango
 
Mama wa watoto mapacha Eliud na Elikana, Grace Joel akiwa amempakata mtoto Eliud ambaye kwa sasa anasumbulia na tatizo la kutokwa na utumbo. Picha na Godfrey Kahango

Utumbo wa mtoto huyo umetoka nje kupitia tundu lililoachwa na madaktari jirani na kitovu chake kwa ajili ya kutolea haja kubwa.

Mwananchi ilishuhudia mtoto huyo akiwa katika hali mbaya na wazazi wa watoto hao, Grace Daud na Erick Mwakyusa walisema walimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Kyela lakini walielezwa kwamba wasubiri kwenda India walikowafanyia upasuaji ili wakarekebishe.

Mwakyusa alisema hivi sasa wanaishi naye kwa kudra za Mwenyezi Mungu na kwamba wanasubiri suala hilo la kwenda India tu.
 
0 comments: