RAIS KIKWETE NA WASANII WETU NI DAM DAM



Utakubaliana na mimi kwamba Rais wetu wa JYMWT Jakaya M Kikwete ni kati ya maraisi wacheche wenye mapenzi mema na wasanii wetu (wa bongo). Mara kadhaa amekuwa akionesha kushirikiana nao katika nyakati mbalimbali. Baadhi ya mambo hayo ni kama ushiriki wake katika kifo cha Kanumba, Bi Kidude n.k.
Pia mara kadhaa Rais amekuwa akiwaita wasanii Ikulu na kubadilishana nao mawazo.

Hivi karibuni Diamond amemshukuru Rais huyo kwa kuonesha kuthamini wasanii wa Tanzani. Kupiti fb Diamond ameandika hivi 


“Wapi Utapata Rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa Thamani ambao unatafutwa karibu na kila mtu Duniani..akautumia kukusaidia kukukutanisha na kukuconnect na Mdau mkubwa Duniani katikaa tasnia uliyopo, ili kuhakikisha tu Unafikia Malengo na Ndoto ya kazi zako.... Dah! Asante sana Mh Rais, Mwenyez Mungu akuzidishie na kukusimamia katika uongozi wako na siku zote za Maisha yako”

HONGERA SANA RAIS WETU KWA KUTHAMINI SANAA YA NYUMBANI

0 comments: