MAZISHI YA MTOTO NASRA YAFANYIKA,BABA MZAZI WA MTOTO AKATAZWA KUMZIKA MWANAYE AISHIA KUAGA TU

Hatimaye
Mtoto Nasra Mvungi aliyefariki Juni mosi mwaka huu kufuatia kuishi
katika mateso makubwa kutoka kwa mama yake mkubwa baada ya mama yake
kufariki na kuishi katika boksi bila huduma muhimu anazostahili kupatiwa
binadamu hasa mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amezikwa kwa
heshima zote na wakazi wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel
Nkaya Bendera, Mbunge wa Morogoro mjini, Abdulaziz Abood na
mfanyabiashara wa mabasi na vituo vya mafuta mkoani Morogoro Al Saed
Omary.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, ametaka vyombo vya sheria Mahakani, kutoa hukumu
inayowastahili waliohusika kwa mateso na kupelekea kifo cha Nasra.
Waombolezaji wakiwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kuaga mwili wa mtoto Nasra Mvungi.
Mfanyabiashara, Al Saed Omary aliyefanikisha kuleta mwili wa marehemu Nasra kutoka Dar es Salaam.
Waombolezaji wakiingia katika mabasi ya Abood, kwenda katika maziko.
Mazishi ya mtoto Nasra yakiendelea makaburi ya Kola mkoani Morogoro.
Mbunge
Abdulaziz Abood akiweka udongo katika kaburi la marehemu Nasra na
kuahidi kumfanyia hitma baada ya siku 40 tangu kuzikwa kwake.
Mfanyabiashara Al Saed Omar nae akiweka udongo katika kaburi la marehemu.
RASHID
Mvungi, baba mzazi wa mtoto Nasra (4), aliyefariki dunia katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, alikolazwa kutokana na
maradhi yaliyokuwa yakimkabili yanayosadikiwa kuchochewa na mateso
aliyoyapata alipokuwa akiishi kwenye boksi kwa takribani miaka minne,
ameshindwa kumzika mwanae katika makaburi ya Kola, Manispaa ya
Morogoro.
Kushindwa
kwake kuhudhuria kuweka undogo katika kaburi la mwanae ni baada ya
kuzuiwa na Polisi kwenda makaburini kwa madai ya kumwepusha na hatari ya
hasira za wananchi kwa unyama waliomfanyia Narsa na walezi wake
wawili.
Baba
mzazi huyo, licha ya awali kushiriki kwenda Jijini Dar es Salaaam
kuuchukua mwili wa mwanaye pamoja na viongozi wa Idara ya Ustawi wa
Jamii Mkoa na Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia, pia alikuwepo uwanja
wa Jamhuri wa Mjini hapa kushiriki shughuli za kuangwa kwa mwili wa
mtoto huyo.
Mvungi
alikuwa ameketi mstari wa mbele ya jeneza la mwanaye wakati wote wa
kutolewa nasaha mbalimbali za viongozi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa,
Joel Bendera na wale wa dini wakiendesha sala ya kabla ya mwili
kuondolewa kwenda msikitini kusaliwa.
Hata hivyo mara baada ya kumalizika shughuli hiyo Mvungi alichukuliwa na Askari Polisi wa kitengo cha Upelelezi Mkoa.
Akihojiwa
na Mwandishi, eneo la Makaburi ya Kola, juu ya kutoonekana kwa baba
mzazi wa marehemu, Narsa, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa,
Kibona, alisema kuwa, isingekuwa jambo la busara kuruhusu Mvungi
ashiriki mazishi makaburini kutokana na kuhofia hasira za wananchi.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa, kuwa Mvungi
aliondolewa uwanjani hapo kwa ajili ya kulinda usalama wake mara baada
ya kumalizika kwa shughuli za kuangwa kwa mwanaye.
NA John Nditi, Morogoro








0 comments: