Naibu Waziri awataja Nay wa Mitego, Shilole, Wema na Aunt Ezekiel kati ya waliopewa onyo na serikali.
Ukiukwaji
wa maadili ni sehemu ya kilio cha jamii ya watanzania na tayari kilio
hicho kimeifikia serikali ambayo imechukua hatua za awali ya kuwaonya
watu wanaofanya tabia hizo.
Naibu
Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia ameeleza
hatua ambazo wizara hiyo imechukua katika kukomesha ukiukwaji wa maadili
unaofanywa hasa katika kumbi za starehe.
Akijibu
swali lililoulizwa na mbunge Catherine Magige, Nkamia amesema kuwa
serikali imefanya vikao na wamiliki wa kumbi za starehe, wamiliki wa
bendi, maafisa wa utamaduni, na wakuu wa polisi.
Amesema
serikali imezuia kutoa vibali kwa vikundi vya ‘Kangamoko’ kutokana na
uchezaji wake kutofuata maadili na kutoa mfano wa wasanii ambao wamepewa
onyo.
“Mfano wasanii waliopewa onyo ni Nay wa Mitego, Shilole na Anti Ezekiel. Na kwa upande wa kumbi ni Mamas &Papas.” Amesema
Naibu
waziri huyo ameeleza kuwa serikali imeunda kamati ya kitaifa yakuzuia
ukatili, unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na watoto na pia
udhalilishaji wa wanawake.
0 comments: