MBASHA ATUPWA RUMANDE HATIMAYE MUME WA FLORA MBASHA ATUPWA RUMANDE

MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora
Mbasha, amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na
mashitaka mawili likiwemo la ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda
makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo
la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha
sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa
kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la
Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa
alimuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.
Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na
wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka
taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa
rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.
Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika
basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya
mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.
0 comments: