RAIS KIKWETE ATUMIA DAKIKA 15 KUMFAGILIA MSANII MKALI DIAMOND
Rais Jakaya Kikwete akimpa mkono wa pongezi Msanii mkali katika miondoko ya Bongo Fleva, Abdul Nassib, Diamond kwa hatua aliyofikia.
Rais
Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza
Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa
alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo
niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”
Diamond (kushoto) akiwa na mkali mwingine wa muziki kutoka Nigeria, maarufu kwa jina la Davido (aliye mbele pichani).
“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete.
Diamond
alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache
baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa
Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa
kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani
hatapata chochote.
0 comments: