MTOTO MWINGINE WA AJABU AZALIWA HUKO SINGIDA,KICHWA TEPE TEPE,KIMEBONYEA BONYEA
Mwanamke
mmoja mkazi wa Kintinku, Wilayani Manyoni mkoani Singida
amejikuta akimwaga machozi baada ya kujifungua mtoto mwenye
kichwa cha ajabu ( tepe tepe).
Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika hospitali ya Kintinku Health Center iliyopo Wilayani Manyoni.....
Akiongea
kwa sharti la kutotajwa jina lake kwa madai kuwa yeye si
msemaji wa hospitali hiyo, Mkunga mmoja wa hospitali hiyo
amedai kuwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika
hatua za mwisho kujifungua.
"Alifikishwa
hapa akiwa katika hatua za mwisho . Hakuwa na kadi yoyote
ya Clinic kwa kuwa hakuwahi kuhudhuria Clinic tangu abebe
mimba hiyo.
"Pamoja
na kutokuwa na kadi ya Clinic, tulianza kumsaidia kujifungua,
lakini mtoto aliyezaliwa alikuwa ni wa tofauti kidogo na
alikuwa amefariki dunia.Kichwa chake kilikuwa tepetepe na
kimebonyea bonyea.
"Ilikuwa
ni ngumu kwetu kutambua tatizo alilokuwa nalo mama huyo kwa
kuwa hakuwa na kadi yoyote ya Clinic ambayo ingeweza
kutusaidia kujua maendeleo ya mtoto huyo alipokuwa tumboni ", alisema Mkunga huyo.
Mwandishi
wa habari hizi alifanya mahojiano na mama huyo ambaye naye
alionyesha kushangazwa na tukio hilo na kusema hajui tatizo
lililomfanya ajifungue mtoto huyo kwa kuwa hakuwahi kusikia
maumivu ya aina yoyote wakati wa ujauzito huo hadi alipofikia
hatua ya kujifungua....
Katika mahojiano hayo, mama huyo alisema kuwa huo ni uzao wake wa 6 na hajawahi hudhuria Clinic
via>>Mpekuzi

0 comments: