MWENYEKITI WA CCM MKOA WA GEITA ANUSURIKA KUPIGWA NA WANANCHI,AJIFICHA KICHAKANI
![]() |
| Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Geita Joseph Msukuma akiwahutubia wananchi wa Geita juzi |
KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Geita
Joseph Msukuma amenusurika kupigwa na wananchi wa katoro akiwa na baadhi
ya viongozi wenzake na kuokolewa na jeshi la polisi baaada ya kufika
kwenye eneo la ujenzi wa vibanda vya serikali ya kijiji hicho na kuamuru
waache ujenzi huo.
Tukio
hilo limetokea leo majira ya asubuhi akiwa anaelekea wilayani Chato
ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya chama ambapo baada ya kufika
kijijini hapo alienda kwenye eneo hilo na kuwakuta mafundi wanajenga
akaanza kuwazuia huku akisema kuwa
..... “ tangu Jumamosi nilitoa maelekezo ya kusitisha ujenzi huu imenibidi nifike mimi mwenyewe nasema muache mara moja".
Baada ya kufika hapo wananchi waliokuwa eneo hilo walianza kuhamasishana na kusema kuwa......
"Mwenyekiti huyu amezoea kutuburuza watu wa Geita mjini, kwa hapa atuache sisi tuendelee na ujenzi"
Baada
ya muda mfupi umati wa wananchi ulikusanyika haraka sana na kumzingira
kwa nia ya kutaka kumpiga kwani hawakufurahishwa na kitendo hicho.
Hata
hivyo baada ya kuona hali imekuwa tete Msukuma alitoweka na kwenda
kujificha kwenye kibanda cha jirani ili kujinusuru asipigwe na umati
uliokuwa umekusanyika wakionekana na hasira huku baadhi ya viongozi
aliokuwa nao walianza kutoweka katika mazingira ya utata.
Mwenyekiti
wa serikali ya kijiji cha Katoro Joeli Mazemle ameulizwa na mwandishi
akasema kuwa ujenzi huo unaoendelea hapo umefuata utaratibu wote kuanzia
ngazi ya kijiji.
"Tunashangaa
Msukuma alipofanya mkutano hapa siku ya Jumamosi akasema kuwa ujenzi
huo usitishwe kwa sababu chama kimesema bila kuainisha tatizo ni
nini",alieleza mwenyekiti wa kijiji
Juhudi za kumpata mwenyekiti wa ccm mkoa wa Geita hazikuzaa matunda kwa sababu alikuwa anaendelea na ziara wilayani Chato .
Baada ya kuwa amenusurika kipigo , simu yake haikuweza kupatikana ili kujua kwa undani kuhusu sakata hilo.
Hivi
karibuni halmashauri ya mji wa Geita wamekuwa na mgogoro baada ya
kuzuia ujenzi wa choo cha soko kuu hadi kikahamishiwa nje kidogo ya mji
eneo la Nyankumbu huku Msukuma akimwita mwenyekiti wa halmashauri hiyo
kuwa ni mwehu katika mkutano wake wa hadhara wa juzi uliofanyika mjini
Geita.
Na Valence Robert- Malunde1 blog Geita

0 comments: