WAZUNGU NOMA, WAMETENGENEZA NDEGE INAYOTUMIA NGUVU YA JUA NA TAYARI IMEANZA KURUKA ANGANI, ITAZAME HAPA
Ndege inayoendeshwa kwa kutumia nguvu ya jua ya Solar Impulse 2 aircraft ambayo ni ya pili katika mfululizo wa ndege za aina hiyo zinazotengenezwa nchini Uswizi leo imeanza safari yake ya kwanza kutoka katika kiwanja chake Magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa watengenezaji, Ndege hiyo ambayo kwa asilimia kubwa
inategemea nguvu ya jua ilipaa angani kwa takribani saa mbili na dakika
15 na kufanikiwa kuruka umbali wa mita 2400.
Kabla ya kufanya majaribio ya toleo hilo la pili, marubani wa ndege
hiyo André Borschberg na Bertrand Piccard walitumia muda mwingi katika
toleo la kwanza la ndege kama hiyo iliyopaa Ulaya hadi Moroco na kupitia
nchini Marekani mwaka 2010 kwa muda wa saa 26 bila kutua.
Baada ya muda mrefu wa majaribio na maandalizi, Watengenezaji hao na
marubani wamefanikiwa kuirusha ndege ya pili leo kwa kutumia jua pekee
ambapo ilitua saa mbili baadae.
Solar Impulse 2 ni kubwa zaidi ya ile ya kwanza lakini ina uzito mdogo ukilinganisha na baadhi ya magari.
Viti vya ndege hiyo vinaweza kulala ambapo sehemu ngumu zaidi itakuwa
ni kukatisha katika bahari za Atlantic na Pacific safari inayoweza
kuchukua siku tano mchana usiku.
Sasa jiulize ikianza kutumika kupandisha abiria utakuwa tayari kupanda?
0 comments: