Dr. Irenius Kapoli enzi za uhai wake
Habari
zilizoufikia mtandao huu wa malunde1 blog zinasema kuwa aliyekuwa
mhadhiri mwandamizi katika chuo kikuu cha Dar es salaam(Shule Kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma-SJMC) Dr Ireneus Kapoli
amefariki dunia leo (Jumamosi)alfajiri.
Chanzo chetu cha habari kimeiambia malunde1 blog kuwa Dr Kapoli amefariki dunia katika hospitali ya Tumbi huko Kibaha kutokana na BP na Kisukari.
Alikimbizwa hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Taarifa
zinasema kuwa msiba uko nyumbani kwake Mbezi (Malamba mawili) jijini
Dar es salaam na mazishi yanatarajia kufanyika kesho kutwa siku ya Jumatatu hapo nyumbani kwake.
Dr
Kapoli alikuwa mtaalam wa lugha ya Kiingereza na alifanya PHD yake
nchini Uingereza ,alianza kufundisha Main Campus Mlimani baadaye
kuajiriwa katika Shule Kuu ya Uandishi wa habari na Mawasiliano ya
Umma(sjmc).
Alifundisha kwa muda wa zaidi ya miaka 10 hapo UDSM-SJMC,akiwa katika idara ya Lugha na alistaafu rasmi mwaka jana.
Mbali na kufundisha smjc Dr Kapoli aliwahi kufanya kazi maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kozi
alizopata kuzifundisha katika chuo hicho enzi za uhai wake ni
"Communications Skills( English for Journalists/Media),"Critical
Discourse Analysis" na "Critical Thinking and Argumentation"
Dr Kapoli alikuwa mtanashati,mpenda haki,mshauri mzuri,mwalimu
bora, mwenye msimamo hakupenda upumbavu hata kidogo,,hakika
aliyefundishwa na mwalimu huyu atakumbuka mengi mema ya Dr Kapoli.
Hata mkurugenzi wa blog hii ya Malunde1 ndugu Kadama Malunde alifundishwa na Dr Kapoli wakati akiwa mwanafunzi katika chuo hicho mwaka 2008/2011. |
0 comments: