KIJANA ALIYEOZA MGUU BAADA YA AJALI, AOMBA MSAADA!!!
Kijana Peter Sitiwati akiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na kuoza kwa mguu.
AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26), mkazi
wa Sinza ya Kwaremmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji
maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar
juzikati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari
mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.
’’Baada ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti
kwenye mguu wa kulia. Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na
baada ya muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda
kilikuwa kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
“Mwanzoni mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi
unatoka sehemu mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana
umeoza tena una matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi
kukaa jirani na mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.
Muonekano wa mguu wa Peter Sitiwati.
Peter alisema atashukuru kama atapata fedha kwa ajili ya matibabu.
“Ila namshukuru sana msamaria mwema anaitwa Louis, ndiye anayenisaidia kwa sasa,” alisema.
Aliongeza kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi ya watu walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
Aliongeza kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi ya watu walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
“Napenda kuwaomba Watanzania mnaosoma Magazeti Pendwa ya Shigongo
mnichangie pesa ili nipate matibabu. Wenye kukuguswa na tatizo langu
wanaweza kunisaidia kwa kutumia namba ya simu
0 comments: