MAUAJI YA KUTISHA KAHAMA..!! MUME ALIYEMALIZA KIFUNGO CHA MIAKA 6 JELA, AMUUA MKEWE KWA WIVU WA MAPENZI
Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
Mkazi
wa Kijiji cha Mpunze Kata ya Mpunze wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Mariam Michael (40) amefariki dunia kwa kupigwa na kitu kizito kichwani
na Mume wake Shija Mandi (45) baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tano usiku wakati wawili hao wakiwa nyumbani kwao.
Amesema chanzo cha awali cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi na kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya uchunguzi.
Katika hatua nyingine Kamugisha amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake watumie vyombo vya sheria katika kutatua migogoro.

Awali
mtuhumiwa Mandi alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa la
unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo ametumikia kifungi hicho na
kuachiliwa huru Ijumaa iliyopita.

0 comments: