PDATE: PICHA TATU ZA BAHATI BUKUKU AKIWA HOSPITALINI BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA YA GARI

Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati
Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi
cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya
gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma
saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi.
Katika ajali hiyo ambayo Bahati
alikuwa akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa
gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT
7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya
miguu na hawezi kutembea.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni
wacheza shoo wa Bahati, Frank Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake
halikupatikana mara moja.
Alfajiri ya juzi, mwandishi wa habari
hizi alimpigia simu Bahati na kuongea naye kuhusu ajali hiyo ambapo huku
akisikika kama anayepata tabu kwa maumivu, alisema:
“Ni kweli tumepata ajali,
nimeumia mgongoni, dereva ameumia mguu. Namshukuru Mungu. Sijui nini
kilitokea, nilishtukia kuona gari kubwa mbele yetu likituvaa, mara
nikashtukia tuko porini. Lakini kabla ya safari Dar tulifanya maombi
makubwa, najua Mungu ametunusuru na kifo kibaya,” alisema Bahati.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa hii si mara ya
kwanza kuripotiwa kwa ajali za magari mkoani Dodoma zikiwahusisha watu
wa tasnia Injili Bongo.
Aprili, mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni
ya Msama Promotion, Alex Msama alipata ajali mbaya ya gari kwa kugongana
na mwendesha bodaboda.Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Ipagala Mwisho,
kilomita chache kabla ya kufika mjini Dodoma. Msama alikuwa kwenye gari
lake aina ya Toyota Mark II GX 100.
Katika ajali hiyo, Msama na mwendesha
bodaboda huyo waliumia sehemu mbalimbali za mwili na kukimbizwa
Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.
Kabla ajali ya Msama haijapoa, Mei,
mwaka huu, Edson Mwasabwite naye alipata ajali kwenye Barabara Kuu ya
Dodoma–Morogoro. Alikuwa akitoka Dodoma kurudi Dar. Alinusurika.
0 comments: