MKE AMCHOMA MUMEWE NA MAJI YA MOTO, KISA WIVU WA MAPENZI
Stori: Haruni Sanchawa
MWANAMKE
mmoja aliyejulikana kwa jina la Fatuma Said mkazi wa Kitunda, Ilala
jijini Dar es Salaam anashikiliwa na Polisi baada ya kummwagia maji ya
moto mumewe sehemu za siri na tumboni kwa kile kinachodaiwa kuwa ni
wivu wa kimapenzi, tukio lililotokea Julai 16 mwaka huu, huko Kitunda.
Chanzo
chetu cha habari kililiambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea saa
12.30 jioni baada ya mwanaume huyo, Adam Rashid ambaye ana wake
wawili, kwenda katika nyumba anayoishi mke mkubwa akiwa ameandamana na
mke mdogo, kwa lengo la kupata maji ya kuoga na kubadili nguo, akitokea
kituo kidogo cha Polisi Stakishari, ambako aliwekewa dhamana kwa
shauri lililokuwa likimkabili.
Inadaiwa
kuwa baada ya kuwekewa dhamana hiyo, Adam na mkewe mdogo, Aisha Juma,
waliamua kwenda nyumba anayoishi mke mkubwa, ambayo inamilikiwa na
mwanaume huyo, kwa ajili ya kuoga na kubadili nguo, wakiamini kuwa
kusingekuwa na matatizo yoyote kwa vile wanawake wote wawili anaishi
nao kihalali na wanafahamiana.
Inasemekana
kuwa baada ya kufika nyumbani hapo, Adam alimtaka mwanaye kumwandalia
maji ya kuoga na akimaliza apewe bukta, ili aweze kuondoka na mke mdogo
kuelekea wanakoishi, lakini wakati hayo yakifanyika, bi mkubwa alianza
kutoa maneno machafu ya kejeli, yaliyoonyesha wazi kuwa alikuwa na
wivu wa kimapenzi.
Majeraha ya maji ya moto aliyopata Bw. Adam Rashid.
Baada
ya mwanaume huyo kumaliza kuoga na kutoka nje, inadaiwa mkewe mkubwa
alijitokeza akiwa amebeba sufuria iliyokuwa na maji ya moto,
yanayodaiwa kuwa yalitakiwa kutumika kwa ajili ya kupikia wali na
kumwagia tumboni na sehemu za siri, huku akiendelea kumtolea maneno ya
kashfa.
MAJERUHI ALONGA NA UWAZI
Akiwa amelazwa katika wodi namba tatu kwenye hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, majeruhi Adamu Rashid alisema Julai 16 mwaka huu alienda nyumbani kwake akiwa ameandamana na mke wake mdogo, lakini akashangazwa na kitendo cha bi mkubwa kuanza kubwata na kumwuliza alichokifuata, kana kwamba amesahau kama pale ni kwake na wote ni wake zake.

“Baada
ya kunimwagia maji, mke wangu mdogo alilia sana kwa uchungu, majirani
wakanichukua na kunipeleka Polisi ambako tulimkuta bi mkubwa akiwa
anaandikisha maelezo kuwa mimi nimempiga, kuona vile askari walimgeuzia
kibao na kumwingiza ndani kwa ajili ya mahojiano zaidi.”
MKE MDOGO NAE
“Ndugu mwandishi, mimi na mume wangu tulienda hadi kwa mke mkubwa bila wasiwasi maana na mimi pale ni kwangu kwa sababu nyumba ya mume wangu halali, lakini tulipofika tuliambulia maneno machafu na kejeli.

Mke
mkubwa alihoji kwa jeuri kitu gani tulichokifuata pale, mume wangu
alikuwa akimjibu kuwa hapa nipo kwangu na huyu niliyekuja naye ni mke
wangu halali, mbona unanifanyia mambo ambayo siyaelewi, yule
hakuelewa, aliendelea tu na maneno yake machafu.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Ilala, SACP Marieth Minagi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa huyo anashililiwa katika kituo cha polisi Wilaya ya kipolisi Ukonga na amefunguliwa jalada na kupewa namba RB/STK/9438/2014 KUJERUHI na uchunguzi unaendelea.

0 comments: