MWANAFUNZI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA MKOKOTENI UNAOVUTWA NA NG'OMBE AKIDANDIA
Mwanafunzi
wa darasa la kwanza wa shule ya msingi Galanzala wilayani Iramba,
amekufa papo hapo baada ya kugongwa na mkokoteni wa kuvutwa na ng'ombe,
uliokuwa ukiongoza na baba yake mlezi.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa ajali hiyo ni ya juzi saa 3:00 asubuhi katika kijiji
cha Uwanza wilayani Iramba.
Kamwela
alisema mkokoteni huo, ambao ulikuwa ukiongozwa na baba mlezi wa mtoto
huyo, Samwel Napegwa ulikuwa umepakia miwa kutoka kijiji cha Galanzala
na ulipofika kijijini hapo ulimgonga mwanafunzi huyo wakati akijaribu
kudandia nyuma.
Alisema
kuwa baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kudandia kikamilifu, aliteleza
kisha kuingia kwenye uvungu wa mkokoteni huo na hivyo kukanyagwa hadi
kifo chake.
Kamwela
alisema uchunguzi wa awali, unaonesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa mwongoza mkokoteni huo, ambaye alishindwa kumzuia mwanafunzi
huyo kudandia mkokoteni.
Kamanda huyo alisema Napegwa alitoroka na kukimbilia kusikojulikana baada ya kutokea ajali hiyo.
0 comments: