Pichani ni Askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ kitengo cha Mabomu wakiwa
katika eneo la tukio ambapo bomu lilirushwa ndani ya Mgahawa ujulikanao
kwa jina la Traditional Indian Cusine uliopo pembeni ya hotel ya Gymkana
jijini Arusha,aidha taarifa za awali zinaeleza kuwa watu nane
wamejeruhiwa vibaya na mlipuko huo .
Picha
ni majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea katika mgahawa wa Traditional
Indian Cusine aliyejulikana kwa jina la Deepak Gupta (25),akiwa amelazwa
katika hospitali ya Selian,katika chumba cha watu mahututi (ICU),mara
baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto kutokana na mhuu huo
kujeruhiwa vibaya na bomu.
Asubuhi
ya leo askari Polisi na wa Jeshi wameizingira nyumba ya Serikali ya
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo iliyopo jirani na Mahakama Kuu
Arusha wakijaribu kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kikiwa kimetegwa
katika geti la kuingilia nyumba hiyo na watu wasiojilikana.
HatA kinjia kinachokatiza maeneo hayo kutokea Mt Meru Hotel nacho kimefungwa kwa muda.
Wakati
huo huo kuna taarifa za usiku zikieleza watu kadhaa wamejeruhiwa katika
Mgahawa mmoja maeneo ya Gymkhana Jijini hapa na wawili kati yao wako
katika hali mbaya.
Hili litakuwa tukio la sita kutokea katika Jiji la Arusha ndani ya muda mfupi, kuanzia May 2013 mpaka sasa.
Tukio la kwanza lilikuwa Kanisani Olasiti watu watatu wakafa.
Baadee katika Mkutano Chadema Soweto watu watatu wakafa tena na mamia kulemaa.
Ikafuata Usa River siku ya Mkesha wa mwaka mpya kwa wamama waliokuwa wanatoka kanisani
Halafu katoka Bar ya Arusha Night Park
Juzi hapa ikawa kwa nyumbani kwa Sheikh maeneo ya Majengo
Na sasa katika hiyo Vama Restaurant na chupuchupu kulipua nyumbani kwa RC!
0 comments: