AMWAGIWA MAHARAGE YA MOTO KISA KUFUMANIWA NA MUME WA MTU
Mke
wa mtu, Mwajuma Prima amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya
kumwagiwa mwilini sufuria la maharage yalitokuwa yakichemka jikoni, kisa
kupeleka maneno ya umbeya kwa mume wa mtu.
Tukio
hilo la kusikitisha lilijiri juzikati majira ya saa 12:00 jioni ambapo
mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Fatuma ndiye anayehusishwa na msala
huo uliotokea nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Ndege, Msamvu mjini
Morogoro.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kwamba, siku ya tukio, Fatuma
alimshutumu Mwajuma kuwa amekuwa akimwambia mumewe maneno ya umbeya ili
kuwatenganisha.
“Huyu Mwajuma anaishi Kihonda, kila baada ya siku tatu anakuja kwenye nyumba hii kumsalimia mama yake mdogo.
“Juzi Fatuma aligombana sana na mumewe na chanzo cha ugomvi huo ilidaiwa kuna mambo mwanaume huyo aliambiwa na Mwajuma.
“Mwajuma alipofika kwa mama yake mdogo ndipo Fatuma akamkwida na kumuuliza kwa nini alimwambia mumewe mambo ya umbeya?
“Mabishano
yalishika kasi na mwishowe walipigana. Fatuma alipoona amezidiwa,
akaingia jikoni na kuipua sufuria la maharage yaliyokuwa yakichemka na
kumwagia Mwajuma mwilini,” alisema mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Akizungumza na mwandishi, mama mdogo wa Mwajuma alisema:
“Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.
“Fatuma alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza kupigana.
“Fatuma ni ndugu yetu, tunatoka naye kijiji kimoja Turiani. Ni kweli alimmwagia Mwajuma maharage ya moto mwilini.
“Fatuma alikuwa anamshutumu mwanangu kumchonganisha na mumewe ndipo walipoanza kupigana.
“Fatuma
alipoona kazidiwa aliingia jikoni akaipua sufuria la maharage
yaliyokuwa yakichemka wna kummwagia mwanangu mwilini na kumsababishia
majeraha makubwa.”
Mume
wa Mwajuma, Peter Muhanda alikiri mkewe kupatwa na masaibu hayo na
kwamba alitoa taarifa polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa.
0 comments: