POLISI WASAKA WAGONJWA WA EBOLA MTAANI
Kituo
maalum kilichotengwa kwa ajili ya kuwaangalia watu wenye dalili za
ugonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia kimeshambuliwa na
watu wasiojulikana waliopora vifaa.
Kwa
mujibu wa BBC, tukio hilo lilifanyika usiku wa Jumamosi iliyopita na
watu takribani 30 walioliokuwa wamewekwa katika kituo hicho kwa lengo la
kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka.
Polisi
wa Monrovia wameingia mitaani kuwasaka watu hao waliotoroka kwa lengo
la kuwarudisha katika kituo hicho huku msako mwingine ukiwa wa kuwasaka
waliotekeleza tukio hilo.
Waandishi
wa habari walioko nchini humo wamesema inawezakana watu waliotekeleza
tukio hilo walichukizwa na kitendo cha serikali kuweka kituo hicho
katika mtaa wao.
Watu
zaidi ya 400 wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia
pekee, na katika kanda ya Afrika Magharibi ni zaidi ya watu 1,000.
0 comments: