BREAKING NEWS..!! MABASI MAWILI YAGONGANNA TABORA NA KUJERUHI ZAIDI YA 50 NA WENGINE 17 KUFA
Watu zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi
ya 50 kujeruhiwa baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katika
kijiji cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 jioni
baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV
lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na
basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa
likitokea Mwanza kupitia Mpanda.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.
Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika
kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na
kufa papohapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa
zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi (Day-worker)

Baadhi ya miili ya marehemu.Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo
ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline
lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Jitihada za kumpata Kamanda wa
Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda
ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.

0 comments: