MTO WA AJABU UPO HANDENI TANGA, KUNA NYOKA MWENYE MASIKIO, MASHARTI UKIFIKA PIGA HODI MARA 3
Utunzaji
wa mazingira ni jukumu la kila mtu kwa pale anapoishi na maeneo yote
yanayomzunguka kwa kuhahakisha kuwa maeneo yanabaki katika uasilia wake.
Suala
la uharibifu wa mazingira linazidi kuenea kila sehemu na kuathiri
misitu,vyanzo vya maji na maeneo mbalimbali ya asili yaliyopo katika
makazi.
Uharibifu
huu wa mazingira unadaiwa kuwa umechangia kupotea kwa asili katika
Kijiji cha Kwedikabu Kata ya Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga
kwani Mto wa ajabu umeanza kukauka.
Kwa
wakazi wa kijiji hiki mto huu ulikuwa muhimu kwani ulikuwa ukitoa maji
baridi na pia pamoja na ukame wa eneo hilo, ulifurika mwaka mzima.
“Hili
eneo lilikuwa halikauki maji ila leo hii yamekauka, tatizo ni hawa
Wamang’ati wanaingiza ng’ombe na kusababisha mizimu kukasirika na
kukausha maji yao. Hapa haparuhusiwi kufanya shughuli yoyote zaidi ya
kuchota maji tu,”anasema mmoja wa wakazi wa kijiji hicho
aliyejitambulisha kwa jina moja Mgaza.
Hamisi Luhezi (55) anaelezea historia ya Mto Mgulwi na kusema kuwa tangu anazaliwa aliukuta na kamwe hakuwahi kuuona ukikauka.
Anasema
kila baada ya miaka mitatu wazee walikwenda eneo hilo na kuchinja
ng’ombe ambapo nyama yake huliwa hukohuko na hakuna mtu atakayeruhusiwa
kwenda nayo nyumbani.
Luhezi
anasema ndani ya msitu huo kuna nyoka mkubwa ambaye ndiye anaelinda
msitu na vyanzo nya maji ila wanahisi kwasasa atakuwa ametoweka ama kufa
kutokana na mazingira ya mto na msitu huo kuharibiwa na shughuli za
kibinadamu.
“Hapa
mtoni kuna nyoka mkubwa anaeitwa Mzimuwachesa, walikuwa wawili na kazi
yao ni kulinda maji lakini hawa Wamang’ati tayari wamemuua mmoja hali
ambayo ilileta kutoelewana miongoni mwa wanakijiji, lakini tayari hatua
stahiki zimechukuliwa kwa wazee kutafuta ng’ombe na kwenda kumchinjia
mtoni kwa minajili ya kutoa sadaka ya kuomba msamaha kwa kosa
hilo,”anasema Luhezi.
Akielezea
masharti ya mto huo, Luhezi anasema ni lazima kila anaekwenda mtoni
apige hodi mara tatu ndio aingie na kwamba hakuna atakaeitikia ila ni
lazima kufanya hivyo.
Anasema
kuwa kuwa majira ya mchana huwa kuna mwali (Malikia) huwa anakuja kuoga
hivyo ni muhimu sana muda huo kupiga hodi endapo utakwenda na hujapiga
hodi ukimkuta utaumwa ama kufa hapo hapo kwani haruhusiwi kuonwa na
binadamu.
“Hurusiwi
kuingia katika mto huo bila ya kupiga hodi mara tatu hasa unapoingia
eneo hilo kuanzia saa sita za mchana, utakapopiga hodi hakuna
atakaeitikia lakini ndio unaruhusiwa kuingia… na ukiingia bila kupiga
hodi unaweza kumkuta mwali (malkia) anaoga au kapumzika akikwambia
kwanini umeingia bila ya kupiga hodi basi huwezi kupona utaugua sana au
kufa kabisa”
Mashariti ya kuingia mtoni
Unapoingia
ndani ya mto Mgulwi muda wa saa 6:00 mchana ni lazima upige hodi kama
ilivyoelezwa awali kuwa ndani ya eneo hilo kuna wenyewe (mizimu) ambao
ndio wanaotunza eneo hilo hivyo usipopiga hodi unaweza kupoteza maisha
au kuugua sana.
Mwisho
wa kuingia mtoni hapo ni saa 12:00 jioni baada ya hapo hakuna
mwanakijiji anaeruhusiwa kuingia tena hadi kesho yake na ukikaidi
yatakayokukuta ni kupoteza maisha msituni humo, ama kusikia au kuona
vitu vya ajabu.
Masharti yaliyowekwa
Kabla ya uvamizi wanakijiji walijiwekea masharti mbalimbali ambayo kutoruhusiwa kuchota maji na sufuria chafu yenye masizi.
Pia
kwa bahati mbaya ukimchota samaki unatakiwa kumrudisha mtoni haraka
iwezekanavyo la sivyo atatoa harufu mbaya ambayo sio ya kawaida na maji
uliochota yote yatageuka kuwa damu.
Hakukuwa
na ruhusa ya kukata mti eneo hilo na ikitokea ukikata mti unapotea njia
ya kurudi nyumbani hadi utupe mti ulioukata ndio fahamu itakurudia na
kuifahamu njia ya kurudi nyumbani.
Mzee Luhezi anasema kwasasa hali ya msitu huo imekuwa mbaya na baadhi ya maajabu yamepungua.
Serikali ya kijiji yazungumza
Akielezea
kuhusu tatizo la uharibifu wa mazingira katika eneo hilo Ofisa Tarafa
wa Kwamsisi, Baraka Hassan anasema kuwa ni kweli kuna uharibifu wa
mazingira katika eneo hilo.
Baraka
anasema kuwa kutokana na hiyo tayari ameshawaagiza watendaji wa kata
kutenga maeneo maalumu kwaajili ya wakulima na wafugaji.
Je bado kuna maajabu?
Afisa tarafa huyo anadai kuwa bado kuna maajabu kwani kuna samaki ambao hawaliwi kwa imani kuwa ukimla unakufa.
Pia yupo nyoka mwenye masikio licha ya kuwa huonekana kwa nadra.
0 comments: