MJANE WA KAMANDA BARLOW AFUKUZWA KWA MAPANGA
Mke wa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Liberates Barlow (53), Stella Barlow (wa
pili kulia) akiomboleza katika mazishi ya mume wake.
UONEVU!
Ikiwa imepita takribani miaka miwili tangu aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mwanza, ACP Liberates Barlow (53) (picha ndogo) afariki dunia
usiku wa Oktoba 13, 2012 kwa kupigwa risasi na watu waliodhaniwa ni
majambazi, mke wa marehemu, Stella Barlow naye yamemkuta mazito kwani
chupuchupu auawe.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Jumatano ya Agosti 13, mwaka huu mjane huyo
anayeishi jijini Mwanza alikwenda Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro
kwenye kaburi alilozikwa mumewe kwa ajili ya kulijenga lakini cha ajabu
ndugu wa marehemu walimfukuza kwa mapanga na marungu na kumtaka aondoke
eneo hilo mara moja.
Chanzo
kilisema kuwa, ndugu hao walimfukuza huku wakidai kwamba awalipe pesa
kwa ajili ya eneo hilo la kaburi alilozikwa mumewe kwa vile marehemu
hakuzikwa kwenye eneo lake, jambo ambalo ilidaiwa kuitia aibu familia
hiyo.
Makamanda wa Polisi wakitoa heshima za mwisho wakati wa mazishi ya ACP Liberates Barlow.
Uwazi
lilimsaka msemaji wa ukoo bila mafanikio lakini mtu mmoja aliyedai si
msemaji akiomba kuhifadhiwa jina lake alisema kilichotokea ni mwanamke
huyo kutaka kuonesha anajua sheria wakati ukoo ulitaka kila kitu kiende
kwa uzuri na utaratibu.
“Sisi
hatukuwa na nia mbaya, kila mtu anajua mila za Kilimanjaro, sasa
tulitaka kuweka mambo sawa, yeye akawa anataka kutuonesha anajua
sheria,” alisema mtu huyo.
Juzi, Uwazi lilimsaka kwa njia ya simu mjane wa marehemu huyo ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:
Juzi, Uwazi lilimsaka kwa njia ya simu mjane wa marehemu huyo ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:
“Ni
kweli tukio hilo lilitokea nilikwednda kwenye kaburi la mume wangu kwa
ajili ya kufanya maombi lakini nilizuiliwa na ndugu wakisema kwamba
hawataki kuniona kwa sababu mume wangu alizikwa pale kimakosa.
“Hata hivyo, walinitimua huku wengine wakinitishia kwa mapanga lakini sijachukua hatua yoyote ila nimemwachia Mungu.”
0 comments: