KIJANA AUAWA KWA KUCHOMWA MO
Mwili wa kijana huyo ukiwa katika gari la polisi kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kijana anayesadikiwa
kuwa kibaka na ambaye hajafahamika jina lake, leo asubuhi amechomwa
moto hadi kufa akidaiwa kuiba baiskeli maeneo ya Nane Nane mjini
Morogoro, jirani na shule ya Sekondari ya Alfa James ambayo ni maarufu
kama Shule ya Father Pekupeku.
”Majira
ya saa moja asubuhi tumeona vijana wanne wakimfukuza mwenzao,
walipofika hapa kwenye mabweni ya shule ya Alfa, wakamkamta akiwa na
baiskeli na kumshushia kichapo kikali na baadaye wakamchoma moto wakidai
alikuwa ameiba baiskeli yao maeneo ya Tubuyu, ” alisema shuhuda mmoja
ambaye alijitambulisha kwa jina la Mama Happy.
Gari la polisi likiondoka na mwili wa kijana huyo.
Kijana
huyo amechomwa moto akituhumiwa kuiba baiskeli kuukuu yenye thamani ya
shilingi 60,000. Polisi walifika na kuuchukua mwili huo na kuupeleka
Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Wanafunzi wa Sekondari ya Alfa James wakishuhudia mahali alipochomewa mtuhumiwa.
0 comments: