Maandamano
yaliyotangazwa na Chadema mkoa wa Shinyanga yaliyopangwa kufanyika leo
saa mbili asubuhi,yameishia pasipojulikana baada ya viongozi wa Chama
hicho kufunga ofisi yao na kutojulikana walipokuwa na baada ya kutafutwa
na waandishi wa habari kujua kulikoni hawaonekani wakati wametangaza
kuandamana,mwenyekiti wa chama hicho mkoa Peter Machanga alidai kuwa leo
walikuwa wanawaandaa tu wananchi kwa ajili ya maandamano
yatakayotangazwa rasmi.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Shinyanga
mjini walisema huenda maandamano hayo yamesitishwa kutokana na askari wa
jeshi la polisi kutapakaa mitaani kwa ajili ya kukabiliana na yeyote
mwenye kujitokeza kuandamana.
Pichani ni ofisi ya Chadema ikiwa imefungwa leo |
0 comments: