ALIYEUAWA KIKATILI NCHINI MAREKANI AZIKWA KWA MAJONZI MKOANI KWAO MOROGORO
MAMIA ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakiongozwa
na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude
wamejitokeza kumzika marehemu Method Clecence Mengi aliyeuawa kwa
kuchomwa visu na watu wasiofahamika nchini Marekani.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude akiuombea mwili wa marehemu Method Clecence Mengi.
Mara baada ya tukio hilo, mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi
kwenda hospitali kwa uchunguzi mpaka Oktoba 1, mwaka huu ulipotolewa na
kuletwa nchini kwa mazishi.
Mwili wa Mengi aliyeishi nchini Marekani tangu mwaka 2000, uliwasili nyumbani kwa wazazi wake, alfajiri ya Oktoba 2, mwaka huu na baadaye saa tisa alasiri kupelekwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Patrick kwa ibada ya mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Marehemu alizikwa saa kumi kwenye Makaburi ya Kolla huku akiacha
maswali ya namna alivyouawa na mkewe ambaye ni Mmarekani kutoonekana
kwenye mazishi wala kuja Bongo.
Akizungumza baada ya mazishi hayo, mdogo wa marehemu Ribbon Mkali ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilakala alisema:
Mengi alikumbwa na ukatili huo wa kuchomwa
visu vitatu, tumboni viwili na kwenye paji la uso Septemba 17, mwaka huu
nje ya nyumba yake, Texas nchini humo na watu hao bila kujulikana kisa
na waliingia mitini baada ya tukio hilo la kikatili.
Mwili wa Mengi aliyeishi nchini Marekani tangu mwaka 2000, uliwasili nyumbani kwa wazazi wake, alfajiri ya Oktoba 2, mwaka huu na baadaye saa tisa alasiri kupelekwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Patrick kwa ibada ya mazishi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Akizungumza baada ya mazishi hayo, mdogo wa marehemu Ribbon Mkali ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilakala alisema:
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
0 comments: