WANACHAMA 13 WANASHIKILIWA NA POLISI AKIWEMO MBUNGE WA MASWA SILVESTER KASULUMBAYI BAADA YA KUWACHARANGA MAPANGA WANACCM...!!
Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro |
Wanachama sita wa CCM akiwemo katibu
Mwenezi wa chama hicho wilayani Kahama wamejeruhiwa vibaya baada ya kukatwa
mapanga na kundi la watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, katika kata ya
Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea jana Majira ya
sa moja jioni wakati wafuasi hao wa CCM wakitoka katika mkutano wa Hadhara wa
kumnadi mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Ubagwe wilayani
Kahama....
katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa kabisa mkono wake wa kushoto |
Waliojeruhuwa katika tukio hilo ni
katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja
cha mkono wa kulia na Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro ambaye
amekatwa panga usoni.
Wengine ni katibu wa umoja wa vijana
CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa panga kichwani na kukatwa
kabisa mkono wake wa kushoto na dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter
aliyekatwa mapanga Kichwani.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono |
Pia amejeruhiwa Ramadhani Salumu,
ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi aliyejeruhiwa mguuni pamoja na
Subira Nyangusu, huku ikielezwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo walipasua vioo
vya gari la CCM na kuchukua funguo za gari hiyo.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wilaya ya
Kahama, Andrew Emanuel majeruhi hao wamelazwa katika hospital ya wilaya hiyo,
huku Kimaro, Masunga na Peter ambao hali zao ni mbaya wakipelekwa hospitali ya
rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani. |
Imedaiwa katika tukio hilo wafuasi
hao wa Chadema wamepora fedha zaidi ya shilingi milioni moja na laki tatu
kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na simu za mkononi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amesema watuhumiwa 16 wa tukio hilo ambao ni wafuasi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, wanashikiliwa na jeshi la polisi Wilaya ya Kahama.
Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama |
0 comments: