MZEE SMALL NAE AFARIKI DUNIA
Mzee Small afariki Dunia.
Habari za kusikitisha zilizotufikia hivi punde
zinaarifu kuwa Mwigizaji maarufu na mkongwe katika fani ya vichekesho nchini
Tanzania, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (59) amefariki dunia baada
ya kuugua kwa muda mrefu.
Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za
usiku wa Juni 7, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akiongea kwa njia ya simu mke wa marehemu, Bi Fatuma
Saidi, ameithibitishia Blog hii, kuwa Msanii Said Ngamba hatunae.
Bi Said amesema kuwa marehemu mumewe amefikwa na
umauti baada ya hali yake kubadilika jana (Juni 7) asubuhi na kumbikiza
Muhimbili ambako alishinda nae akipatiwa matibabu na majira ya saa tatu usiku
alirudi nyumbani na kumwacha kijana wake akimwangalia mgonjwa na ilipotimu saa
tano usiku kijano huyo alirudi na kusema baba amefariki.
“Nikweli Mzee Small amefariki”….yalikuwa ni
maneno machache yaliyobenba uchungu mzito kufuatia kifo cha mumewe.
Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
Blog ya Wamtomi inatoa pole kwa familia
yake yote, Ndugu jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.

0 comments: