WANAMKE AJITOA MHANGA,AVAMIA KAMBI YA JESHI
Mwanamke aliyejitolea mhanga alijiripua nje ya kambi ya jeshi, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi wawili walijeruhiwa vibaya.
Aliripua bomu wakati akihojiwa na wanajeshi.Afisa wa jeshi aliiambia BBC
kwamba mwanamke huyo aliyevaa hijabu, alikaribia kambi kwa piki-piki
katika jimbo la Gombe.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo,
anasema siyo kawaida kwa mwanamke kushambulia kwa kujitolea mhanga
nchini Nigeria, na jimbo la Gombe limekuwa salama kwa jumla.
Hakuna kundi lilodai kufanya shambulio hilo.
Lakini kundi la Waislamu la Boko Haram, limekuwa likilenga makambi ya jeshi na polisi.
0 comments: