PICHA ZA MAJERAHA ALIYOYAPATA DIDA BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI KUTOKA KWA MUMEWE

Majeraha katika mwili wa Dida baada ya kipigo kutoka kwa mumewe Ezden.
 Picha zinazoonyesha jinsi mtangazaji wa kituo cha Redio cha Times, Khadija Shaibu alivyochezea kichapo kutoka kwa mumewe, Edzen Jumanne zimevuja.
Picha hizo zinamuonesha Dida akiwa na majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mkononi, kichwani na mapajani.
 
Dida Akiwa na Edzen
 
Dida Akiwa na Edzen
 
Akizungumzia kipigo hicho hivi karibuni, Dida alidai kuwa, baada ya kutofautiana kufuatia wivu wa kimapenzi, mume wake huyo baada ya kumporomoshea mitusi, alichukua mkanda wa suruali na kumpiga nao hadi kumsababishia majeraha hayo hali inayomfanya muda mwingi avae kininja kuficha aibu.
 
Dida akionyesha majeraha aliyoyapata.
 
Dida akionyesha majeraha aliyoyapata.
 
Mpaka sasa wawili hao kila mmoja kivyake huku ndoa ikielezwa kuwa haipo tena.

0 comments: