HUYU NDIYO MSHINDI /MISS LAKE ZONE 2014,ANATOKA MKOANI GEITA,NAMBA 2 NA 3 KUTOKA SHINYANGA
Mkurugenzi
wa Lenny Hotel Leonard Bugomola akikabidhi funguo za gari kwa Miss Lake
zone 2014 Rahel Clevery-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Mshindi
wa kwanza/Miss Lake Zone 2014-Rahel Clevery akiwa ameshikilia funguo za
gari la milioni 10 alilopewa kama zawadi ya ushindi-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Hatimaye
kitendawili cha nani atakuwa Miss Lake Zone Mwaka 2014 kwa warembo kumi
na nane (18) kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kimeteguliwa baada ya Rahel
Clevery kutoka Geita kuibuka mshindi na kuondoka na gari lenye thamani
ya Tsh. Milioni Kumi lililotolewa na mkurugenzi wa Lenny Hotel iliyoko
mkoani Geita- Leonard Bugomola.
Mashindano
hayo yamefanyika juzi katika uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza na
kuhudhuriwa na watu wachache ambapo mgeni rasmi alikuwa Leonard
Bugomola ambaye ni mkurugenzi wa Lenny Hotel.
Akiwahutubia
wananchi hao wachache pamoja na warembo hao aliwataka washiriki wa
shindano hilo kuendelea kutunza nidhamu kama walivyoishi kwake kwa
kipindi chote hicho hata watakapokwenda kwenye mikoa yao waendelee kuwa
hivyo kwa kuwaheshimu wote.
Bugomola alishangazwa na kitendo cha watu wa mkoa wa Mwanza kuwa wachache katika viwanja hivyo japokuwa walitangaziwa siku nyingi.
"Jamani mimi, Mgeni rasmi sikutegemea kama watu wa Mwanza watakuwa wachache kiasi hiki ,maana Geita walifurika sana na huku mmetangaziwa kwa kipindi kirefu sana kuhusu shindano hili",aliongeza
Hata
alisema yeye ataendelea kudhamini mashindano mengine na kuomba kibali
kupitia kwa Ashim Lundenga kama itawezekana shindano la Miss Tanzania
mwaka ujao lifanyike mkoani Geita.
Akipokea
zawadi ya Gari hiyo Miss Lake zone 2014 Rahel alisema kuwa atahakikisha
anatangaza vivutio vyote vilivyoko katika mkoa wake na kutoa shukrani
zake kubwa kwa Mkurugenzi wa Lenny Hotel ambaye amekuwa ni msaada mkubwa
kwao kwa kipindi chote cha siku kumi walichokaa kambini kwa kujifunza nidhamu na heshima kwa watu wote.
Mshindi
alioweza kuibuka kidedea katika mashindano hayo ni Rahel Clevery kutoka
Geita, aliyenyakua gari lenye thamani ya Tshs. Mil. 10 lililotolewa
Mkurugenzi wa Lenny Hotel iliyoko Mkoani Geita.
Mshindi
wa pili ni Mary Emmanuel kutoka Shinyanga na mshindi wa tatu ni Nicole
Sarakikya kutoka Shinyanga na mshindi wa nne ni Dorini Robert kutoka Mwanza.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Mwanza


0 comments: